Wednesday, 8 February 2017

MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUFAULU MTIHANI



MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUFAULU MTIHANI
Katika hali ya kawaida kwa nchi yetu ya Tanzania kipimo pekee ambacho huwa kinatumika kumpima mwanafunzi kutoka level moja kwenda nyingine ni mtihani.Bila kufaulu mtihani hutaweza kwenda kwenye level nyingine ya elimu,hivyo kufaulu ni njia pekee ya kukuvusha kwenda level nyingine.Sasa kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa wanafunzi wetu kufaulu mitihani yao.Asilimia kubwa wanaishi kufeli na kushindwa kuendelea na level  nyingine.Yapo mambo ambayo yanaweza kukusaidia kufaulu mtihani kama utayazingatia kwa undani zaidi.Jambo la kwanza kabisa ni kumtanguliza mwenyenzi Mungu mwingi wa rehema ili aweze kukubariki na kukupa afya njema kipindi chote cha mitihani yako kwa sababu kama hutakuwa na afya njema itakuwa kikwazo cha wewe kufanya vizuri katika mitihani yako.Pia hakikisha kile ulichofundishwa na walimu wako au wakufunzi wako unakishika kwa ufasaha zaidi ,hii ni sehemu muhimu sana ambayo inabebeba asilimia kubwa za wewe kufaulu mtihani wako.Kama hutaweza kukishika na kuelewa kile unachofundishwa basi kufaulu kwako mtihani kutakuwa ni ndoto.Ukijaribu kusoma maandiko matakatifu yanasema shika sana elimu  hivyo unapaswa kuvishika vile vyote ulivyovisoma.Pia kumaliza silabasi yako mapema kutakusaidia sana ili upate mda wa kufanya marudio mapema,kama hutamaliza silabasi mapema  hutaweza kupata mda wa kufanya marudio.Hii ni sehemu muhimu sana katika ufaulu wako wa mtihani.Vilevile unapaswa upate mda wa kumpumzika ili akili iweze kupangilia mambo uliyo ya soma.Kumbuka kusoma sio vita au ugomvi unapaswa kurilaksi wakati mwingine .Akili ya mwanadamu ni kama kompyuta wakati mwingine huwa inastaki na unaweza kusahau kabisa baadhi ya mambo kama hutaipumzisha ,hivyo kupumzika ni muhimu sana.Jambo jingine nikujiongeza katika masomo yako ,unapaswa kuhangaika kutafuta rasilimali elimu ili ziweze kukusaidia katika ufaulu wako.Pia kupunguza mambo ambaya sio ya muhimu kwa wakati huo yatakusaidia  kukupa mda zaidi wa kusomaYapo baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuyaepuka wakati wa kusoma ambayo ni mapenzi,ulevi,uvutaji wa sigara na bangi,kwenda kwenye kumbi za strarehe nakadhalika.Nidhamu pia ni jambo la muhimu sana katika ufaulu wako,unapaswa kuwa na nidhamu kwa walimu wako ,wazazi na wote wanaokuzunguka ili uweze kusaidika zaidi.Nidhamu ni muhimu sana hata ukiwa kwenye mtihani .Vilevile unapaswa ufanye mtihani wako kwa umakini mno unapokuwa katika chumba cha mtihani,usikimbilie kutoka nje maana uko nje hakuna majibu,hakikisha unafanya mtihani wako kwa uangalifu mkubwa.Tumia mda vizuri wakati wa kusoma na pia wakati wa kufanya mtihani wako,hakikisha unakimbizana na mda kwenye mtihani wako.Muda ndo uanowagarimu wengi katikaa mitihani kwasababu wanachukua mda mrefu kufikiria majibu ,hivyo unapaswa kuwa  makini sana na muda.Hyo ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia ktika ufaulu wa mtihani wako.Itaendelea

3 comments: