MAMBO YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUFAULU
MTIHANI
Katika hali
ya kawaida kwa nchi yetu ya Tanzania kipimo pekee ambacho huwa kinatumika
kumpima mwanafunzi kutoka level moja kwenda nyingine ni mtihani.Bila kufaulu
mtihani hutaweza kwenda kwenye level nyingine ya elimu,hivyo kufaulu ni njia
pekee ya kukuvusha kwenda level nyingine.Sasa kumekuwa na changamoto kubwa sana
kwa wanafunzi wetu kufaulu mitihani yao.Asilimia kubwa wanaishi kufeli na
kushindwa kuendelea na level
nyingine.Yapo mambo ambayo yanaweza kukusaidia kufaulu mtihani kama
utayazingatia kwa undani zaidi.Jambo la kwanza kabisa ni kumtanguliza mwenyenzi
Mungu mwingi wa rehema ili aweze kukubariki na kukupa afya njema kipindi chote
cha mitihani yako kwa sababu kama hutakuwa na afya njema itakuwa kikwazo cha
wewe kufanya vizuri katika mitihani yako.Pia hakikisha kile ulichofundishwa na
walimu wako au wakufunzi wako unakishika kwa ufasaha zaidi ,hii ni sehemu
muhimu sana ambayo inabebeba asilimia kubwa za wewe kufaulu mtihani wako.Kama
hutaweza kukishika na kuelewa kile unachofundishwa basi kufaulu kwako mtihani
kutakuwa ni ndoto.Ukijaribu kusoma maandiko matakatifu yanasema shika sana
elimu hivyo unapaswa kuvishika vile
vyote ulivyovisoma.Pia kumaliza silabasi yako mapema kutakusaidia sana ili
upate mda wa kufanya marudio mapema,kama hutamaliza silabasi mapema hutaweza kupata mda wa kufanya marudio.Hii ni
sehemu muhimu sana katika ufaulu wako wa mtihani.Vilevile unapaswa upate mda wa
kumpumzika ili akili iweze kupangilia mambo uliyo ya soma.Kumbuka kusoma sio
vita au ugomvi unapaswa kurilaksi wakati mwingine .Akili ya mwanadamu ni kama
kompyuta wakati mwingine huwa inastaki na unaweza kusahau kabisa baadhi ya
mambo kama hutaipumzisha ,hivyo kupumzika ni muhimu sana.Jambo jingine
nikujiongeza katika masomo yako ,unapaswa kuhangaika kutafuta rasilimali elimu
ili ziweze kukusaidia katika ufaulu wako.Pia kupunguza mambo ambaya sio ya
muhimu kwa wakati huo yatakusaidia kukupa mda zaidi wa kusomaYapo baadhi ya mambo
ambayo unapaswa kuyaepuka wakati wa kusoma ambayo ni mapenzi,ulevi,uvutaji wa
sigara na bangi,kwenda kwenye kumbi za strarehe nakadhalika.Nidhamu pia ni
jambo la muhimu sana katika ufaulu wako,unapaswa kuwa na nidhamu kwa walimu
wako ,wazazi na wote wanaokuzunguka ili uweze kusaidika zaidi.Nidhamu ni muhimu
sana hata ukiwa kwenye mtihani .Vilevile unapaswa ufanye mtihani wako kwa
umakini mno unapokuwa katika chumba cha mtihani,usikimbilie kutoka nje maana
uko nje hakuna majibu,hakikisha unafanya mtihani wako kwa uangalifu
mkubwa.Tumia mda vizuri wakati wa kusoma na pia wakati wa kufanya mtihani
wako,hakikisha unakimbizana na mda kwenye mtihani wako.Muda ndo uanowagarimu wengi
katikaa mitihani kwasababu wanachukua mda mrefu kufikiria majibu ,hivyo
unapaswa kuwa makini sana na muda.Hyo ni
baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia ktika ufaulu wa mtihani wako.Itaendelea
Nashukuru nimejifunza kitu kikubwa
ReplyDeleteNmejifunza
ReplyDeleteNashukuru
ReplyDelete