SIFA ZA KIONGOZI
ANAYEFAA
Kiongozi ni mtu
aliyepewa dhamana na jamii au serikali ili aweze kusimamia shughuli mbalimbali
katika iyo jamii au serikali.Zipo baadhi ya sifa ambazo ni lazima kiongozi awe
nazo ili atambulike kama kiongozi.Ikitokea kiongozi hana hizi sifa basi
hastaili kabisa kuwa kiongozi katika jamii au serikali.Baadhi ya sifa hizo ni
hizi zifuztazo
Awaze maono kwa jamii yake:Kiongozi bora lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake, sekta yake inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia wafanyakazi na watendaji wote walio chini yakekatika jamii au serikali ili kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai kuwa kiongozi katika jamii au serikali.
Awe na nia ya kutimiza mambo mbalimbali yanayomuhusu: kiongozi atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.

Ajitambue mwenyewe:Wapo baadhi ya viongozi hawajitambui
kabisa kuwa wao ni viongozi wa serikali
au jamii.Lazima kiongozi ajitambue kuwa yeye ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na
upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili
changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na
ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.
Awe na maamuzi na msimamo:Kuna wakati kiongozi hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwa na msimamo na maamuzi sahihi. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna maanisha udhaifu wa kiongozi huyo.
Akubali kukosolewa:Kiongozi asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake.
Awe msikilizaji:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi wao.
Afuate haki:Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai.
Awe na akiba ya maneno: kiongozi mzuri ni yule ambaye huwa ana akiba ya maneno ,hapayukipayuki ovyovoyo hadharani.Huwa anafikiria cha kuongea ili kisije mgarimu siku moja.Wapo baadhi ya viongozi ambao hawana akiba ya maneno huwa wanaongea kilakitu bila ya kuchagua vitu vya kuongea.

.
Awatie moyo watu:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuwatia moyo watu katika jamii ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao kama wafanyakazi au wananchi.
Afurahie mafanikio:Sifa nyingine muhimu ya kiongozi ni kuwa tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.
Akubali lawama:Kama kiongozi amefanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitengo fulani kwa mfano na watu hawakupata nishuduma kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama.
Afahamu kutatua matatizo:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.
Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.
Hizo ni baadhi ya sifa za kiongozi katika jamii au serikali na kabla mtu hajapewa madaraka lazima jamii au serikali impime kama hizi sifa anazo.

No comments:
Post a Comment