Thursday, 30 March 2017

KUTAMBUA NA KUKUZA KIPAJI CHAKO



KUTAMBUA NA KUKUZA KIPAJI CHAKO
Kipaji ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho pasipo kufundishwa na mtu yeyote.Vipo vipaji vingi ambavyo binadamu anaweza kuwa navyo lakini asigundue mapema kuwa amezaliwa na kipaji hicho.Baadhi ya vipaji hivyo ni kuimba nyimbo,kucheza mziki,ususi,uchongaji wa vinyago,kuigiza,kuchekesha nakadhalika.Ila imekuwa ngumu sana kwa watu wengi kutambua kuwa wamezaliwa na vipaji hivi,na wengi wanakuja kutambua wakiwa wameshakuwa wakubwa.Zipo baadhi ya njia zinazoweza kukusaidia kutambua kipaji chako mapema na ukakikuza na kukiendeleza na mwisho wa siku kikakusaidia kufikia malengo yako  katika maisha.
Njia ya kwanza kabisa ya kutambua kipaji chako ni kufanya kile ambacho unahisi unaweza kukifanya kwa wakati huo.Hii itakusaidia sana kujua kipaji chako mapema kwasababu utakapo anza kufanya kile ambacho unahisi unaweza kufanya unaweza kujikuta umefanikiwa zaidi kuliko ungelikaa kimya bila kukifanya.Kwa mfano kama unahisi unaweza kuimba anza kuimba mapema wakati ukiwa na nguvu  na mwisho wa siku utajikuta unakuja kuwa msanii mzuri sana katika hiyo jamii inayokuzungunga.Wapo baadhi ya wasanii wamejaliwa kugundua kipaji chao mapema na wamefanikiwa kwa kiwango cha juu sana na wanaumri mdogo.
Fanyia mazoezi hicho kipaji chako ambacho unahisi Mungu kakujalia.Hakikisha unaanza mazoezi ili uweze kukikuza hicho kipaji chako ambacho mwenyenzi Mungu amekujali.Mazoezi yataendeleza kipaji chako na kukikuza zaidi kuliko ambavyo ungeamua kukaa kimya bila kufanya mazoezi.
Shirikisha wadau kwenye hicho kipaji chako.Inapendeza sana kama utawashirikisha wadau mbalimbali hasa wenye kipaji kama chako ili nao waweze kukuongezea baadhi ya vitu katika hicho kipaji chako.Wadau watakusaidia sana kwa naamna moja au nyingine kukuza kipaji chako kwasababu sapoti yao kwako ni muhimu sana.Pia unaweza kushirikisha hata mashirika  mbalimbali ambayo yanasaidi kukuza baadhi ya vipaji kwenye jamii.
Njia nyingine ni kutokuwa muoga wakati unapoanza kukiinua kipaji chako.Ukiwa muoga hutaweza kukiendeleza kipaji chako.Unapaswa kuwa jasiri wakati wote na pia uwe mvumilivu kwasababu unaweza ukachukua mda kidogo kukikuza kipaji chako.Hakikisha unajituma vya kutosha na uoga unauweka pembeni kwani uoga huwakwamisha wengi katika kukuza vipaji vyao.
Uwe mbunifu zaidi.Ili kukuza kipaji chako unatakiwa uwe mbunifu sana, unapaswa kujiongeza zaidi ili kipaji chako kiweze kukua.Hakikisha unajiongeza kwa wenzako ili uweze kuchukua baadhi ya vitu kutoka kwao na kuviongeza katika kipaji chako.Kwa kufanya hivi kutakusaidia sana kukiendeleza na kukuza kipaji chako.Ubunifu ndo kila kitu kwenye kiapji chako kama hutakuwa mbunifu zaidi basi itakuwa ngumu kukiendeleza kipaji chako
Pia usikate tama kwa kuwa mafanikio huja taratibu.Usitake mafanikio ya haraka kwani yanaweza kukukwamisha kwasababu endapo hutafanikiwa mapema basi unaweza ukaamua kuachana na kipaji chako na kufanya mambo mengine ambayo yanaweza yakakukwamisha zaidi.Hivyo ni vizuri ukawa mvumilivu na ukapambana taratibu na mwisho wa siku utajikuta umefanikiwa zaidi kuliko kutaka mafanikio ya haraka zaidi.
Unapaswa kuwa na vyanzo vya pesa ili kusaidia kukuza kipaji chako.Pesa ni kitu muhimu sana katika kukuza kipaji chako kwani unaweza hitaji baadhi ya vitendea kazi ukashindwa kuvinunua kwasababu tu huna fedha za kutosha.Hivyo unapaswa kuwa na vyanzo vya fedha ili viweze kukusaidia.Vipo vyanzo vingi vya fedha kama vile kuomba marafiki zako au wadau mbalimbali wakuchangie au kushirikisha mashirika mbalimbali ambayo yanaweza kukusaidia kifedha.Pia unaweza ukashirikisha wazazi wako kama wanaweza kukusaidia kifedha.

Friday, 24 February 2017

UMUHIMU WA KUTUMIA KISWAHILI



UMUHIMU WA KUTUMIA KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania,pia ni lugha ambayo inamtambulisha mtanzania popote duniani lakini inashangaza kuona Kiswahili hakitumiki ipasavo kama lugha ya Taifa letu la Tanzania.Tumekuwa na utamaduni wa kukipuza Kiswahili na kutukuza lugha za kigeni kama kingereza na lugha nyinginezo.Hata katika elimu yetu tumekuwa tukitumia sana lugha za kigeni kuliko kutumia Kiswahili.Kwa mfano katika shule zetu za msingi tumekuwa tukitumia sana Kiswahili.Masomo karibu yote yanafundishwa kwa Kiswahili isipokuwa kwa somo moja tu la kingereza.Hii imefanya watoto wengi kujua lugha ya Kiswahili kwa ufasaha zaidi.Ni ngumu sana kumkuta mwanafunzi kahitimu darasa la saba na hajui kabisa kuzungumza Kiswahili, ila ni rahisi kwa mwanafunzi kuhitimu darasa la saba na akawa hajui kabisa kuzungumza kingereza hata cha kuomba maji.Matumiza ya Kiswahili kwa shule za msingi yamesaidia sana kukuza Kiswahili Tanzania ila inashangaza sana mwanafunzi anapoingia kidato cha kwanza anakutana na masomo tisa  na kati ya hayo tisa moja tu ndo linafundishwa kwa lugha ya Kiswahili na mengine yote nane yana fundishwa kwa kingereza .Hii ni ajabu kubwa sana kwa Tanzania,na kikubwa zaidi walimu wanaomfundisha huyu mwanafunzi pindi anapoingia kidato cha kwanza wanategemea azungumze kingereza,  kamwe huyu mwanafunzi itakuwa ngumu sana kwake kuzungumza kwasababu hakuwa na msingi mzuri wa kingereza  kama ilivo kwa Kiswahili na matokeo yake ni kwamba mwanafunzi huyu atazungumza zaidi Kiswahili kuliko kingereza.Sasa ifike mahali watanzania tujitathimini wenyewe je ni sahihi kutumia lugha ya kingereza na wakati asili yetu sisi sio kingereza bali ni kiswahilii na kama ni sahihi kutumia kingereza basi mitahala ya msingi nayo ibadilike ifundishwe kwa kingereza ili mwanafunzi atakapo ingia kidato cha kwanza aweze kuzungumza kingereza vizuri na kama tumeamua kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo ndo luhga inayomtambulisha Mtanzania basi vilevile mitahala ya sekondari nayo ibadilike ili mwanafunzia anayetoka shule ya msingi ambako wanafundishwa Kiswahili takribani masomo yote aweze kuzungumza kiswhili kizuri.Hakuna nchi duniani ambayo  ina lugha yake ya taifa alafu wanafunzi wake wanafundishwa masomo karibu yote kwa lugha za kigeni,mfano mzuri ni nachi kama marekani ambayo lugha yake ya taifa ni kingereza hata wanafunzi wao wote kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu wanafundishwa kwa lugha yao ya taifa ambayo ni kingereza .Ni Tanzania tu ndo tumekuwa na utanaduni wa kutukuza lugha za kigeni na kupuuza lugha yetu ya Kiswahili ambayo watanzania takribani asilimia 99.9 wanaitumia kwa ufasaha zaidi.Tufike sehemu watanzania tubadiilke na kuanza kutumia lugha ya kiswahili kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.Mda wa kutumia lugha za kigeni umepitwa na wakati tukumbuke kuwa hatuko katika nyakati za ukoloni tena tupo katika nyakati za kuhakikisha kuwa Kiswahili kinakua na nchi nyingine nazo zije zijifunze kutumia lugha ya Kiswahili.Serikali ichukue jukumu la kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika katika kila kona ya Tanzania hii itasidia sana kukuza Kiswahili ,zipo nchi ambazo zimeshaanza kuchukukua hatua na kuhakikisha Kiswahili kinatumika ipasavo,hii itasidia sana kukuza Kiswahili kwa nchi za Afrika.Kiswahili kikitumiwa vizuri kitatuletea faida kubwa sana kama taifa.Faida mojawapo ni kutambulisha nchi za afrika na pia asili ya mwafrika.Vilevile kitasaidia kutambulisha rasilimali na vivutio mabalimbali vilivo Tanzania kama vile madini ya tanzanaiti na hifadhi za mbuga za wanyama.Hivyo naishauri serikali  ishirikishe wadau mbalimbali ili waweze kusaidia kukuza lugha ya Kiswahili.Pia mfumo wetu wa elimu ubadilishwe na tuanze kutumia Kiswahili kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu na kingereza kifundishwe tu kama somo na sio medium of instruction kama ilivo sasa.

Sunday, 19 February 2017

SIFA ZA KIONGOZI ANAYEFAA



SIFA ZA KIONGOZI ANAYEFAA
Kiongozi ni mtu aliyepewa dhamana na jamii au serikali ili aweze kusimamia shughuli mbalimbali katika iyo jamii au serikali.Zipo baadhi ya sifa ambazo ni lazima kiongozi awe nazo ili atambulike kama kiongozi.Ikitokea kiongozi hana hizi sifa basi hastaili kabisa kuwa kiongozi katika jamii au serikali.Baadhi ya sifa hizo ni hizi zifuztazo

Awaze maono kwa jamii yake:Kiongozi bora lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake, sekta yake inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia wafanyakazi na watendaji wote walio chini yakekatika jamii au serikali ili kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai kuwa kiongozi katika jamii au serikali.

Awe na nia ya kutimiza mambo mbalimbali yanayomuhusu: kiongozi atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.

Ajitambue mwenyewe:Wapo baadhi ya viongozi hawajitambui kabisa kuwa wao ni  viongozi wa serikali au jamii.Lazima kiongozi ajitambue kuwa yeye  ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.

Awe na maamuzi na msimamo:Kuna wakati kiongozi  hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kuwa na msimamo na maamuzi sahihi. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna maanisha udhaifu wa kiongozi huyo.

Akubali kukosolewa:Kiongozi asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake.

Awe msikilizaji:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi wao.

Afuate haki:Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai.

Awe na akiba ya maneno: kiongozi mzuri ni yule ambaye huwa ana akiba ya maneno ,hapayukipayuki ovyovoyo hadharani.Huwa anafikiria cha kuongea ili kisije mgarimu siku moja.Wapo baadhi ya viongozi ambao hawana akiba ya maneno huwa wanaongea kilakitu bila ya kuchagua vitu vya kuongea.
.

Awatie moyo watu:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuwatia moyo watu katika jamii ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao kama wafanyakazi au wananchi.

Afurahie mafanikio:Sifa nyingine muhimu ya kiongozi ni kuwa tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.

Akubali lawama:Kama kiongozi amefanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitengo fulani kwa mfano na watu hawakupata nishuduma  kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama.

Afahamu kutatua matatizo:Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.

Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.

Hizo ni baadhi ya sifa za kiongozi katika jamii au serikali na kabla mtu hajapewa madaraka lazima jamii au serikali impime kama hizi sifa anazo.



Friday, 17 February 2017

JITAMBUE: FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI

JITAMBUE: FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI: Imeandikwa na Julius I.Sanare 0757- 012317 www.blogger.com au www.jitambue1.blogspot.com FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI Moja ya mahi...

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI



Imeandikwa na Julius I.Sanare
0757- 012317
www.blogger.com au www.jitambue1.blogspot.com
FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI
Moja ya mahitaji muhimu kwa mwanadamu ni Mazoezi. Mazoezi ni mhimu kwa ajili ya afya pamoja na kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body).Watu wengi huishia kula chakula tu bila kufanya mazoezi, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika. Kwa hiyo mazoezi ni muhimu kama ilivyo kwa maji na chakula katika miili yetu.
Zifuatazo ni faida za kufanya mazoezi.
Ø  Hukufanya ujisikie vizuri
Ø   Huongeza uwezo wa kujifunza
Ø   Hujenga uwezo wa kujistahi
Ø  Huongeza nguvu ya ubongo kufanya kazi
Ø   Huuweka mwili wako kuwa unaofaa (fit) na wenye uwezo
Ø   Huongeza afya ya akili yako
Ø   Huongeza kinga ya mwili
Ø   Hupunguza mfadhaiko/stress
Ø  Hukufanya ujisikie vizuri/mwenye furaha
Ø   Hukufanya usizeeke mapema
Ø   Huweka ngozi yenye mng’aro na yenye afya
Ø  Husaidia kupata usingizi mtulivu
Ø   Husaidia kuzuia ugonjwa wa kiharusi/strokes
Ø   Huongeza ufanisi katika makutano/joints za mwili
Ø  Huongeza nguvu za mishipa
Ø   Huondoa wasiwasi
Ø   Huongeza kumbukumbu
Ø   Husaidia kudhibiti ulevi/uteja
Ø   Huongeza uzalishaji
Ø  Huongeza uwezo wa ubunifu
Ø  Hupendezesha muonekano wa mwili
Ø   Huongeza uwezo wa kujiamini
Ø   Husaidia kuongeza nguvu juu ya malengo yako maishani
Ø   Huondoa tatizo la kukinaishwa na chakula
Ø   Huongeza miaka ya kuishi
Ø   Hukomaza mifupa
Ø   Huongeza afya ya moyo
Ø  Huongeza hali ya kuwa na msimamo
Ø  Huondoa homa ndogo ndogo mwilini
Ø   Huongeza hamu ya kula
Ø  Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa
Ø  Hushusha shinikizo la juu la damu
Ø   Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari
Ø  Huzuia kupatwa na ukichaa/uwendawazimu
Ø   Hupunguza au huzuia maumivu ya mgongo
Ø  Hupunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa mifupa
Ø  Hupunguza hisiaaufikra za kujisikia vibaya au huzuni
Ø  Huzuia kupotea kwa mishipa
Ø  Huongeza nguvu na ustahimilivu
Ø  Huongeza ufanisi katika michezo
Ø   Huongeza uwezo wa kuvumilia maumivu
Ø   Huongeza usawa na ushirikiano wa mwili
Ø  Huongeza usambazaji wa oksijeni katika seli za mwili
Ø   Huongeza hali ya ufuatiliaji
Ø   Huongeza uwezo wa kujitawala na kujidhibiti nafsi
Ø   Huondoa uchovu
Ø   Huongeza nguvu katika tendo la ndoa
Ø   Hufanya maisha yawe kuvutia zaidi
Ø  Huongeza ubora wa maisha
Tujitahidi sana kufanya mazoezi kwani yatatusaidia sana katika kujenga miili yetu.