Friday, 24 February 2017

UMUHIMU WA KUTUMIA KISWAHILI



UMUHIMU WA KUTUMIA KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania,pia ni lugha ambayo inamtambulisha mtanzania popote duniani lakini inashangaza kuona Kiswahili hakitumiki ipasavo kama lugha ya Taifa letu la Tanzania.Tumekuwa na utamaduni wa kukipuza Kiswahili na kutukuza lugha za kigeni kama kingereza na lugha nyinginezo.Hata katika elimu yetu tumekuwa tukitumia sana lugha za kigeni kuliko kutumia Kiswahili.Kwa mfano katika shule zetu za msingi tumekuwa tukitumia sana Kiswahili.Masomo karibu yote yanafundishwa kwa Kiswahili isipokuwa kwa somo moja tu la kingereza.Hii imefanya watoto wengi kujua lugha ya Kiswahili kwa ufasaha zaidi.Ni ngumu sana kumkuta mwanafunzi kahitimu darasa la saba na hajui kabisa kuzungumza Kiswahili, ila ni rahisi kwa mwanafunzi kuhitimu darasa la saba na akawa hajui kabisa kuzungumza kingereza hata cha kuomba maji.Matumiza ya Kiswahili kwa shule za msingi yamesaidia sana kukuza Kiswahili Tanzania ila inashangaza sana mwanafunzi anapoingia kidato cha kwanza anakutana na masomo tisa  na kati ya hayo tisa moja tu ndo linafundishwa kwa lugha ya Kiswahili na mengine yote nane yana fundishwa kwa kingereza .Hii ni ajabu kubwa sana kwa Tanzania,na kikubwa zaidi walimu wanaomfundisha huyu mwanafunzi pindi anapoingia kidato cha kwanza wanategemea azungumze kingereza,  kamwe huyu mwanafunzi itakuwa ngumu sana kwake kuzungumza kwasababu hakuwa na msingi mzuri wa kingereza  kama ilivo kwa Kiswahili na matokeo yake ni kwamba mwanafunzi huyu atazungumza zaidi Kiswahili kuliko kingereza.Sasa ifike mahali watanzania tujitathimini wenyewe je ni sahihi kutumia lugha ya kingereza na wakati asili yetu sisi sio kingereza bali ni kiswahilii na kama ni sahihi kutumia kingereza basi mitahala ya msingi nayo ibadilike ifundishwe kwa kingereza ili mwanafunzi atakapo ingia kidato cha kwanza aweze kuzungumza kingereza vizuri na kama tumeamua kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo ndo luhga inayomtambulisha Mtanzania basi vilevile mitahala ya sekondari nayo ibadilike ili mwanafunzia anayetoka shule ya msingi ambako wanafundishwa Kiswahili takribani masomo yote aweze kuzungumza kiswhili kizuri.Hakuna nchi duniani ambayo  ina lugha yake ya taifa alafu wanafunzi wake wanafundishwa masomo karibu yote kwa lugha za kigeni,mfano mzuri ni nachi kama marekani ambayo lugha yake ya taifa ni kingereza hata wanafunzi wao wote kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu wanafundishwa kwa lugha yao ya taifa ambayo ni kingereza .Ni Tanzania tu ndo tumekuwa na utanaduni wa kutukuza lugha za kigeni na kupuuza lugha yetu ya Kiswahili ambayo watanzania takribani asilimia 99.9 wanaitumia kwa ufasaha zaidi.Tufike sehemu watanzania tubadiilke na kuanza kutumia lugha ya kiswahili kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.Mda wa kutumia lugha za kigeni umepitwa na wakati tukumbuke kuwa hatuko katika nyakati za ukoloni tena tupo katika nyakati za kuhakikisha kuwa Kiswahili kinakua na nchi nyingine nazo zije zijifunze kutumia lugha ya Kiswahili.Serikali ichukue jukumu la kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika katika kila kona ya Tanzania hii itasidia sana kukuza Kiswahili ,zipo nchi ambazo zimeshaanza kuchukukua hatua na kuhakikisha Kiswahili kinatumika ipasavo,hii itasidia sana kukuza Kiswahili kwa nchi za Afrika.Kiswahili kikitumiwa vizuri kitatuletea faida kubwa sana kama taifa.Faida mojawapo ni kutambulisha nchi za afrika na pia asili ya mwafrika.Vilevile kitasaidia kutambulisha rasilimali na vivutio mabalimbali vilivo Tanzania kama vile madini ya tanzanaiti na hifadhi za mbuga za wanyama.Hivyo naishauri serikali  ishirikishe wadau mbalimbali ili waweze kusaidia kukuza lugha ya Kiswahili.Pia mfumo wetu wa elimu ubadilishwe na tuanze kutumia Kiswahili kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu na kingereza kifundishwe tu kama somo na sio medium of instruction kama ilivo sasa.

No comments:

Post a Comment