Saturday, 11 February 2017

SABABU ZA VIJANA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA



SABABU ZA VIJANA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wadogo kujiingiza katika utumiaji na uzaji  wa madawa ya kulevya pasipokujua madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya.Hii imepelekea Taifa kupoteza nguvu kazi kubwa sana kwa sababu vijana ndo Taifa la leo.Badala ya vijana kujikita katika shughuli za maendeleo na kukuza uchumi wao wameamua kujiingiza katikautumiaji na uzaji wa madawa ya kulevya.Zipo sababu ambazo zimewafanya vijana wengi kujiingiza katika wimbi hili la utumiaji wa madawa ya kulevya.Sababu mojawapo ni kupoteza au kupunguza mawazo.Vijana wengi wamekuwa wakijidanganya kuwa pindi watakapo tumia dawa za kulevya kama vile bangi,cocaine watapunguza msongo wa mawazo waliyonayo ila ukweli utabaki palepale kwamba binadamu yeyeto aliyekamilika ni lazima awe na mawazo usipokuwa na mawazo inawezekana kabisa hujakamilika.Hivyo kumia kwako dawa hakuta kupunguzia mawazo kabisa.Pia wengi wanatumia ili waweze kufanya kazi bila kuchoka au kuwaongezea nguvu mwilini pindi wanapokuwa kwenye kazi ngumu lakini mwisho wa siku wanaishia kuwa vichaa na kupata matatizo ya kiafya.Wapo pia ambao wanatumia kwa ajili ya starehe zao,wanahisi wakitumia madawa ya kulevya kunaa mihemko fulani ndani ya miili yao wanaisikia.Vilevile wapo wanotumia kutokana na kushawishiwa na wenzao watumie  ili waweze kupata mafanikio kama waliyonayo wenzao.Lakini ukweli ni kwamba wa kutumia madawa ya kulevya hakuna mafanikio yeyote ambayo utayapata zaidi sana ni kwamba hata yale mafanikio uliyonayo yanaweza yakapotea kutokana na kutumia muda na pesa nyingi kwenye madawa ya kulevya.Vijana wengine wanahisi wakitumia madawa ya kulevya kunaufahari fulani wanaupata,wanahisi kuwa madawa hayana madhara katika miili yao ila madawa ya kulevya huwa yanamadhara makubwa sana kiasi kwamba yanaweza ata kukusitishia maisha yako (kifo) .Nini kifanyike ili kuwaepusha vijana katika janga hili la kutumia madawa ya kulevya.Kwanza kabisa elimu itolewe kwa vijana ili waweze kutambua madhaya yatokayo na matumizi ya dawa za kulevya.Serikali na wadau wa sekta binafsi watoe elimu kwa vijana maana vijana ndo kundi kubwa linaloangamia na janga hili.Vijana wapatiwe elimu ya ujasiria mali ili waweze kujikita katika uzalishaji zaidi kuliko kutumia madawa ya kulevya.Pia vijana wapatiwe mikopo nafuu na serikali pamoja na taasisi binafsi ili waweze kufungua miradi ya kuwaweka bize wasipate mda wa kutumia madawa ya kulevya.Hii itasaidia sana maana kumekuwa na wimbi kubwa sana la vijana wasio na ajira mwisho wa siku wanaamua kutumia madawa ya kulevya angalau kupunguza msongo wa mawazo wa kutokuwa na ajira.Vilevile serikali ianzishe  taasisi za kudili na vijana ili kuhakikisha vijana wanawajibika ipasavyo na si kutumia madawa ya kulevya kama ilivo sasa.Pia vijana wengi wapelekwe JKT kujifunza nidhamu kwasababu wengi wanaotumia madawa hata nidhamu hawana kwasababu mwenye nidhamu na anayejua ananafanya nini kwa wakati gani hawezi kutumia madawa ya kulevya.Pi a vijana wapewe  fursa mbalimbali ambazo zitawawezesha kujikwamua kimaisha.Kama haya yatazingatiwa kwa umakini vijana wanaweza kuepuka kabisa kutumia dawa za kulevya.
Imeandikwa na Julius I. Sanare.
0757- 012317



No comments:

Post a Comment