KUTAMBUA NA KUKUZA
KIPAJI CHAKO
Kipaji ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho pasipo kufundishwa
na mtu yeyote.Vipo vipaji vingi ambavyo binadamu anaweza kuwa navyo lakini
asigundue mapema kuwa amezaliwa na kipaji hicho.Baadhi ya vipaji hivyo ni
kuimba nyimbo,kucheza mziki,ususi,uchongaji wa vinyago,kuigiza,kuchekesha
nakadhalika.Ila imekuwa ngumu sana kwa watu wengi kutambua kuwa wamezaliwa na
vipaji hivi,na wengi wanakuja kutambua wakiwa wameshakuwa wakubwa.Zipo baadhi
ya njia zinazoweza kukusaidia kutambua kipaji chako mapema na ukakikuza na
kukiendeleza na mwisho wa siku kikakusaidia kufikia malengo yako katika maisha.
Njia ya kwanza kabisa ya kutambua kipaji chako ni kufanya
kile ambacho unahisi unaweza kukifanya kwa wakati huo.Hii itakusaidia sana kujua
kipaji chako mapema kwasababu utakapo anza kufanya kile ambacho unahisi unaweza
kufanya unaweza kujikuta umefanikiwa zaidi kuliko ungelikaa kimya bila
kukifanya.Kwa mfano kama unahisi unaweza kuimba anza kuimba mapema wakati ukiwa
na nguvu na mwisho wa siku utajikuta
unakuja kuwa msanii mzuri sana katika hiyo jamii inayokuzungunga.Wapo baadhi ya
wasanii wamejaliwa kugundua kipaji chao mapema na wamefanikiwa kwa kiwango cha
juu sana na wanaumri mdogo.
Fanyia mazoezi hicho kipaji chako ambacho unahisi Mungu
kakujalia.Hakikisha unaanza mazoezi ili uweze kukikuza hicho kipaji chako
ambacho mwenyenzi Mungu amekujali.Mazoezi yataendeleza kipaji chako na kukikuza
zaidi kuliko ambavyo ungeamua kukaa kimya bila kufanya mazoezi.
Shirikisha wadau kwenye hicho kipaji chako.Inapendeza sana
kama utawashirikisha wadau mbalimbali hasa wenye kipaji kama chako ili nao
waweze kukuongezea baadhi ya vitu katika hicho kipaji chako.Wadau watakusaidia
sana kwa naamna moja au nyingine kukuza kipaji chako kwasababu sapoti yao kwako
ni muhimu sana.Pia unaweza kushirikisha hata mashirika mbalimbali ambayo yanasaidi kukuza baadhi ya
vipaji kwenye jamii.
Njia nyingine ni kutokuwa muoga wakati unapoanza kukiinua kipaji
chako.Ukiwa muoga hutaweza kukiendeleza kipaji chako.Unapaswa kuwa jasiri
wakati wote na pia uwe mvumilivu kwasababu unaweza ukachukua mda kidogo
kukikuza kipaji chako.Hakikisha unajituma vya kutosha na uoga unauweka pembeni
kwani uoga huwakwamisha wengi katika kukuza vipaji vyao.
Uwe mbunifu zaidi.Ili kukuza kipaji chako unatakiwa uwe
mbunifu sana, unapaswa kujiongeza zaidi ili kipaji chako kiweze kukua.Hakikisha
unajiongeza kwa wenzako ili uweze kuchukua baadhi ya vitu kutoka kwao na
kuviongeza katika kipaji chako.Kwa kufanya hivi kutakusaidia sana kukiendeleza
na kukuza kipaji chako.Ubunifu ndo kila kitu kwenye kiapji chako kama hutakuwa
mbunifu zaidi basi itakuwa ngumu kukiendeleza kipaji chako
Pia usikate tama kwa kuwa mafanikio huja taratibu.Usitake
mafanikio ya haraka kwani yanaweza kukukwamisha kwasababu endapo hutafanikiwa
mapema basi unaweza ukaamua kuachana na kipaji chako na kufanya mambo mengine
ambayo yanaweza yakakukwamisha zaidi.Hivyo ni vizuri ukawa mvumilivu na
ukapambana taratibu na mwisho wa siku utajikuta umefanikiwa zaidi kuliko kutaka
mafanikio ya haraka zaidi.
Unapaswa kuwa na vyanzo vya pesa ili kusaidia kukuza kipaji
chako.Pesa ni kitu muhimu sana katika kukuza kipaji chako kwani unaweza hitaji
baadhi ya vitendea kazi ukashindwa kuvinunua kwasababu tu huna fedha za
kutosha.Hivyo unapaswa kuwa na vyanzo vya fedha ili viweze kukusaidia.Vipo
vyanzo vingi vya fedha kama vile kuomba marafiki zako au wadau mbalimbali
wakuchangie au kushirikisha mashirika mbalimbali ambayo yanaweza kukusaidia
kifedha.Pia unaweza ukashirikisha wazazi wako kama wanaweza kukusaidia kifedha.
No comments:
Post a Comment