UMUHIMU
WA NIDHAMU:
Imeandikwa
na Julius I.Sanare
+255
0757-012317
www.blogger.com au www.jitambue1.blogspot.com.
Nidhamu ni
uwezo wa kufanya mambo au vitu fulani pasipo kufuata hisia au kinyume na
ulivyozoea.Yapo maeneo muhimu ambayo yanahitaji nidhamu ya hali ya juu.Baadhi
ya maeneo hayo ni nidhamu ya kufikiri
vizuri, nidhamu ya kutunza muda,nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii, nidhamu ya
kujitunza kiafya,nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza, nidhamu ya ujasiri au
ushujaa na nidhamu ya kujifunza.
Nianze na nidhamu ya kufikiri vizuri.Kufikiri ni
jambo la muhimu sana katika maisha ya kawaida ya mwanadamu,na kufikiri huku
kunaenda sambamba na nidhamu.Nidhamu ya kufikiri vizuri husaidia kupunguza kutoa
maneno ambayo hayastaili katika mazingira fulani,kwa maana nyingine nidhamu ya
kufikiri husaidia kuwa na akiba ya manenno ya kusema mbele za watu.Mtu ambaye
hana nidhamu ya kufikiri huwa anapayuka tu ili mradi amezungumza.
Eneo lingine ni nidhamu ya kutunza muda.Tukumbuke
kuwa muda ndo kilakitu katika maisha yetu ya kila siku.Kama hatutakuwa na nidhamu ya kutunza muda vizuri basi kuna
siku itatugarimu.Muda ndo pesa na maisha ni muda ndo maana siku zinavozidi
songa mbele kama kuna mambo hujayakamilisha basi inawezekana ukagaramika uko
mbeleni.Hivyo ni lazima tuwe na nidhamu ya muda.
Pia tunapaswa tuwe na nidhamu ya kufanya kazi kwa
bidii.Siku zote kazi yeyote ile inahitaji nidhamu ili uweze kufanikiwa kuifanya
iyo kazi kwa umakini.Kama hutakuwa na nidhamu katika kazi basi hutaiheshimu iyo
kazi yako na haitakaa ikusaidie kwasababu
huna nidhamu na kazi yako.Hivyo tujitahidi kuwa na nidhamu katika kazi
zetu za kila siku na pia tuziheshimu,na tukumbuke msemo usemao heshima ni kazi.
Vilevile tuwe na nidhamu ya kujitunza
kiafya.Tukumbuke kuwa ili uweze kuishi vizuri unapaswa kuwa na afya njema,na
ili uwe na afya njema nidhamu inahitajika pia.Afya njema ni muhimu sana kwa
maisha ya binadamu ya kila siku,kama
hutakuwa na nidhamu uwezekano wa kutokuwa na afaya njema ni mkubwa kwasababu hutaweza
kujizuia baadhi ya mambo ambayo ni atari kwa afya lakini kama unanidhamu basi
utakuwa na afya njema.
Pia tunapaswa kuwa na nidhamu ya kuweka akiba na
kuwekeza.Uwekezaji ni muhimu sana katika maisha,bila kuwekeza hutaweza
kufanikiwa katika maisha.Akiba huwa inasaidia sana ila nidhamu inahitajika
katika uwekezaji, kama hutakuwa na nidhamu basi uwekezaji wako utakuwa wa ovyo.
Mwisho pia tunapaswa kuwa na nidhamuya kujifunza mambo
mbalimbali ambayo yatatusaidi katika maisha yetu.Elimu na nidhamu huwa vinaenda
sambamba na ndo maana tunasisistizwa tuwe na nidhamu ili tuweze kulisaidia
taifa letu
SPELLING MISTAKES AND ERRORS
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDeleteNzuri boresha uandishi wako
ReplyDeleteI give it 32/40
ReplyDeleteWell written thanks I have learnt something
ReplyDeleteI give it 38/40. Well done writer
ReplyDeleteNingempa 29/40 kwasababu ya 'spelling Israel'skarma Anaya Au maneno
ReplyDeleteSafi sana 38/40
ReplyDelete