Monday, 30 January 2017

ZIJUE SABABU ZA WANAUME KUTOKUOA NA WANAWAKE KUTOKUOLEWA



ZIJUE SABABU ZA WANAUME  KUTOKUOA NA WANAWAKE KUTOKUOLEWA
Katika maisha ya kawaida tunayoishi hakuna mwanamke asiyependa kuolewa au mwanaume asiyependa kuoa ila zipo baadhi ya sababu ambazo huwa zinamfanya mtu afikie hatua ya kuamua kutokuoa au kutokuolewa kabisa.Niaze na upande wa wanaume.Vijana wengi wa kiume sikuizi hawataki kabisa kusikia swala zima la kuoa nahii ni kutokana na sababu mbalimbali ambazo nitazieleza katika makala hii.Sababu moja wapo ambayo imekuwa ikichangia vijana wengi wa siku izi wasioe ni kutaka uhuru ili waweze kutoka kimapenzi na wasichana mbalimbali.Hii inatokana na kwamba vijana wengi wanahisi wakioa watabanwa sana na wake zao hivyo watakosa uhuru wa kujiachia na wasicha wa aina tofauti tofauti,na ndo maana hawaitaji kabisa suala la kuoa na ikitokea mwanamke akamtajia neno kuoa basi inakuwa rahisi kwa mwanaume kumuacha na kutafuta mwanamke mwingine.Sababu nyinge ni ugumu wa maisha,wanaume wengi wamekuwa wakilalamika kuwa maisha ni magumu hivyo hawawezi kuoa kwasababu watakuwa wanazidi kijiongeze kizingiti cha maisha. Wengi wamekuwa wakifikiri labda kuna maisha mengine marahisi totauti na hayo wanayoishi kwa sasa.Ukweli ni kwamba  maisha hayo unayoishi sasa yanaweza yasibadilike sana kama hutafanya jitihada binafsi na inawezekana ukaoa na ukawa na maisha mazuri sana kuliko ambayo ulikuwa nayo kabla hujaoa kwasabau unapoamua kuoa kunabadhi ya majukumu yataongezeka hivyo itakubidi uongeze juhudi zaidi katika maisha ili uweze kufikia malengo yako.Sababu nyingine ni vijana  kudai wanajipanga kimaisha,ukweli utabaki palepale kuwa maisha tunayoishi hayana fomula kamili isipokuwa ni wewe mwenyewe kuyapeleka utakavo ili uweze kutimiza ndoto zako.VIjana wengi wamekuwa wakidai kuwa bado wanajipanga kimaisha  ndo waweze kuoa ila ukweli wala hakuna wanacho jipanga bali ni kukwepa swala zima la kuoa.Pia wapo vijana wengine wanahisi wakioa watakuwa wamepoteza kabisa dira ya maisha kwasababu wanawachukilia wanawake kama kikwazo katika maisha yao.Ila kama utaishi vizuri na mkeo hawezi kuwa kiwazo chochote katika maisha yako.Hizo ni baadhi tu ya sababu ambazo huwa zinawafanya wanaume wengi wasioe kabisa ila pia kwa upande wa wanawake zipo pia sababu ambazo zinawafanya wasiolewe kabisa.Sababu mojawapo ni baadhi ya wanawake kutohitaji kabisa kuzaa hivyo wanaona hawana sababu ya wao kuolewa na wanaamua kuishi maisha yao binafsi.Na ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anayetaka kuoa mwanamke ambaye hayuko tayari kumzalia watoto.Sababu ya pili ya wanawake kutoolewa ni kwamba wanawake wengi wanahisi wakiolewa watanyanyasika kwa wanaume zao ila si mkweli kwamba watanyanyasika iispokuwa kila mmoja anapaswa kumuheshimu mwenzie ili waweze kwenda sawa katika maisha ambayo wameamua kuishi pamoja.Kama mtakuwa na mtazamo tofauti basi kutofautiana kutakuwepo ila isiwe ni sababu ya kutoolewa.Pia wanawake wengine hawaolewi kwasababu wamekuwa wakijirahisha kwa wanaume zao kipindi wanapokuwa katika mahusiano ya awali na inafikia hatua mwanaume anamuona hana jipya kwasababu amesha mpa kilakitu hivyo anaona hata akimuoa hakuna cha zaidi atakachokuja kukipata maana ameshapewa vyote pindi wakiwa katika mahusiano ya ujana,hivyo wanawake wanapaswa wajitafakari mara mbilimbli kwa wanaume zao wasijiachie ikapitiliza.Pia wanawake wengi  wamekuwa  wakihitaji kuwa huru,hawataki kubanwabanwa na wanaume zoa ndo maana hawataki kabisa swala zima la kuolewa.Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazowafanya wanaume wasioe na wanawake wasiolewewe.

No comments:

Post a Comment