Wednesday, 15 February 2017

UMUHIMU WA NIDHAMU



UMUHIMU WA NIDHAMU:
Imeandikwa na Julius I.Sanare
+255 0757-012317
www.blogger.com au www.jitambue1.blogspot.com.
Nidhamu ni uwezo wa kufanya mambo au vitu fulani pasipo kufuata hisia au kinyume na ulivyozoea.Yapo maeneo muhimu ambayo yanahitaji nidhamu ya hali ya juu.Baadhi ya maeneo hayo ni nidhamu ya kufikiri vizuri, nidhamu ya kutunza muda,nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii,  nidhamu ya kujitunza kiafya,nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza, nidhamu ya ujasiri au ushujaa na nidhamu ya kujifunza.
Nianze na nidhamu ya kufikiri vizuri.Kufikiri ni jambo la muhimu sana katika maisha ya kawaida ya mwanadamu,na kufikiri huku kunaenda sambamba na nidhamu.Nidhamu ya kufikiri vizuri husaidia kupunguza kutoa maneno ambayo hayastaili katika mazingira fulani,kwa maana nyingine nidhamu ya kufikiri husaidia kuwa na akiba ya manenno ya kusema mbele za watu.Mtu ambaye hana nidhamu ya kufikiri huwa anapayuka tu ili mradi amezungumza.
Eneo lingine ni nidhamu ya kutunza muda.Tukumbuke kuwa muda ndo kilakitu katika maisha yetu ya kila siku.Kama hatutakuwa  na nidhamu ya kutunza muda vizuri basi kuna siku itatugarimu.Muda ndo pesa na maisha ni muda ndo maana siku zinavozidi songa mbele kama kuna mambo hujayakamilisha basi inawezekana ukagaramika uko mbeleni.Hivyo ni lazima tuwe na nidhamu ya muda.
Pia tunapaswa tuwe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii.Siku zote kazi yeyote ile inahitaji nidhamu ili uweze kufanikiwa kuifanya iyo kazi kwa umakini.Kama hutakuwa na nidhamu katika kazi basi hutaiheshimu iyo kazi yako na haitakaa ikusaidie kwasababu  huna nidhamu na kazi yako.Hivyo tujitahidi kuwa na nidhamu katika kazi zetu za kila siku na pia tuziheshimu,na tukumbuke msemo usemao heshima ni kazi.
Vilevile tuwe na nidhamu ya kujitunza kiafya.Tukumbuke kuwa ili uweze kuishi vizuri unapaswa kuwa na afya njema,na ili uwe na afya njema nidhamu inahitajika pia.Afya njema ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu  ya kila siku,kama hutakuwa na nidhamu uwezekano wa kutokuwa na afaya njema ni mkubwa kwasababu hutaweza kujizuia baadhi ya mambo ambayo ni atari kwa afya lakini kama unanidhamu basi utakuwa na afya njema.
Pia tunapaswa kuwa na nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza.Uwekezaji ni muhimu sana katika maisha,bila kuwekeza hutaweza kufanikiwa katika maisha.Akiba huwa inasaidia sana ila nidhamu inahitajika katika uwekezaji, kama hutakuwa na nidhamu basi uwekezaji wako utakuwa wa ovyo.
Mwisho pia tunapaswa kuwa na nidhamuya kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatatusaidi katika maisha yetu.Elimu na nidhamu huwa vinaenda sambamba na ndo maana tunasisistizwa tuwe na nidhamu ili tuweze kulisaidia taifa letu
 






8 comments: