UMUHIMU WA KUTUMIA
KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania,pia ni lugha
ambayo inamtambulisha mtanzania popote duniani lakini inashangaza kuona
Kiswahili hakitumiki ipasavo kama lugha ya Taifa letu la Tanzania.Tumekuwa na
utamaduni wa kukipuza Kiswahili na kutukuza lugha za kigeni kama kingereza na
lugha nyinginezo.Hata katika elimu yetu tumekuwa tukitumia sana lugha za kigeni
kuliko kutumia Kiswahili.Kwa mfano katika shule zetu za msingi tumekuwa
tukitumia sana Kiswahili.Masomo karibu yote yanafundishwa kwa Kiswahili
isipokuwa kwa somo moja tu la kingereza.Hii imefanya watoto wengi kujua lugha
ya Kiswahili kwa ufasaha zaidi.Ni ngumu sana kumkuta mwanafunzi kahitimu darasa
la saba na hajui kabisa kuzungumza Kiswahili, ila ni rahisi kwa mwanafunzi
kuhitimu darasa la saba na akawa hajui kabisa kuzungumza kingereza hata cha
kuomba maji.Matumiza ya Kiswahili kwa shule za msingi yamesaidia sana kukuza
Kiswahili Tanzania ila inashangaza sana mwanafunzi anapoingia kidato cha kwanza
anakutana na masomo tisa na kati ya hayo
tisa moja tu ndo linafundishwa kwa lugha ya Kiswahili na mengine yote nane yana
fundishwa kwa kingereza .Hii ni ajabu kubwa sana kwa Tanzania,na kikubwa zaidi
walimu wanaomfundisha huyu mwanafunzi pindi anapoingia kidato cha kwanza
wanategemea azungumze kingereza, kamwe
huyu mwanafunzi itakuwa ngumu sana kwake kuzungumza kwasababu hakuwa na msingi
mzuri wa kingereza kama ilivo kwa
Kiswahili na matokeo yake ni kwamba mwanafunzi huyu atazungumza zaidi Kiswahili
kuliko kingereza.Sasa ifike mahali watanzania tujitathimini wenyewe je ni
sahihi kutumia lugha ya kingereza na wakati asili yetu sisi sio kingereza bali
ni kiswahilii na kama ni sahihi kutumia kingereza basi mitahala ya msingi nayo
ibadilike ifundishwe kwa kingereza ili mwanafunzi atakapo ingia kidato cha
kwanza aweze kuzungumza kingereza vizuri na kama tumeamua kutumia Lugha ya
Kiswahili ambayo ndo luhga inayomtambulisha Mtanzania basi vilevile mitahala ya
sekondari nayo ibadilike ili mwanafunzia anayetoka shule ya msingi ambako
wanafundishwa Kiswahili takribani masomo yote aweze kuzungumza kiswhili
kizuri.Hakuna nchi duniani ambayo ina
lugha yake ya taifa alafu wanafunzi wake wanafundishwa masomo karibu yote kwa
lugha za kigeni,mfano mzuri ni nachi kama marekani ambayo lugha yake ya taifa
ni kingereza hata wanafunzi wao wote kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu
wanafundishwa kwa lugha yao ya taifa ambayo ni kingereza .Ni Tanzania tu ndo
tumekuwa na utanaduni wa kutukuza lugha za kigeni na kupuuza lugha yetu ya
Kiswahili ambayo watanzania takribani asilimia 99.9 wanaitumia kwa ufasaha
zaidi.Tufike sehemu watanzania tubadiilke na kuanza kutumia lugha ya kiswahili
kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.Mda wa kutumia lugha za kigeni umepitwa
na wakati tukumbuke kuwa hatuko katika nyakati za ukoloni tena tupo katika
nyakati za kuhakikisha kuwa Kiswahili kinakua na nchi nyingine nazo zije
zijifunze kutumia lugha ya Kiswahili.Serikali ichukue jukumu la kuhakikisha
kuwa Kiswahili kinatumika katika kila kona ya Tanzania hii itasidia sana kukuza
Kiswahili ,zipo nchi ambazo zimeshaanza kuchukukua hatua na kuhakikisha
Kiswahili kinatumika ipasavo,hii itasidia sana kukuza Kiswahili kwa nchi za
Afrika.Kiswahili kikitumiwa vizuri kitatuletea faida kubwa sana kama taifa.Faida
mojawapo ni kutambulisha nchi za afrika na pia asili ya mwafrika.Vilevile
kitasaidia kutambulisha rasilimali na vivutio mabalimbali vilivo Tanzania kama
vile madini ya tanzanaiti na hifadhi za mbuga za wanyama.Hivyo naishauri
serikali ishirikishe wadau mbalimbali
ili waweze kusaidia kukuza lugha ya Kiswahili.Pia mfumo wetu wa elimu
ubadilishwe na tuanze kutumia Kiswahili kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu
na kingereza kifundishwe tu kama somo na sio medium of instruction kama ilivo
sasa.
No comments:
Post a Comment