ZIJUE SABABU ZA
WANAUME KUTOKUOA NA WANAWAKE KUTOKUOLEWA
Katika maisha ya kawaida tunayoishi hakuna mwanamke
asiyependa kuolewa au mwanaume asiyependa kuoa ila zipo baadhi ya sababu ambazo
huwa zinamfanya mtu afikie hatua ya kuamua kutokuoa au kutokuolewa kabisa.Niaze
na upande wa wanaume.Vijana wengi wa kiume sikuizi hawataki kabisa kusikia
swala zima la kuoa nahii ni kutokana na sababu mbalimbali ambazo nitazieleza
katika makala hii.Sababu moja wapo ambayo imekuwa ikichangia vijana wengi wa
siku izi wasioe ni kutaka uhuru ili waweze kutoka kimapenzi na wasichana
mbalimbali.Hii inatokana na kwamba vijana wengi wanahisi wakioa watabanwa sana
na wake zao hivyo watakosa uhuru wa kujiachia na wasicha wa aina tofauti
tofauti,na ndo maana hawaitaji kabisa suala la kuoa na ikitokea mwanamke
akamtajia neno kuoa basi inakuwa rahisi kwa mwanaume kumuacha na kutafuta
mwanamke mwingine.Sababu nyinge ni ugumu wa maisha,wanaume wengi wamekuwa
wakilalamika kuwa maisha ni magumu hivyo hawawezi kuoa kwasababu watakuwa
wanazidi kijiongeze kizingiti cha maisha. Wengi wamekuwa wakifikiri labda kuna
maisha mengine marahisi totauti na hayo wanayoishi kwa sasa.Ukweli ni
kwamba maisha hayo unayoishi sasa
yanaweza yasibadilike sana kama hutafanya jitihada binafsi na inawezekana ukaoa
na ukawa na maisha mazuri sana kuliko ambayo ulikuwa nayo kabla hujaoa kwasabau
unapoamua kuoa kunabadhi ya majukumu yataongezeka hivyo itakubidi uongeze
juhudi zaidi katika maisha ili uweze kufikia malengo yako.Sababu nyingine ni
vijana kudai wanajipanga kimaisha,ukweli
utabaki palepale kuwa maisha tunayoishi hayana fomula kamili isipokuwa ni wewe
mwenyewe kuyapeleka utakavo ili uweze kutimiza ndoto zako.VIjana wengi wamekuwa
wakidai kuwa bado wanajipanga kimaisha
ndo waweze kuoa ila ukweli wala hakuna wanacho jipanga bali ni kukwepa
swala zima la kuoa.Pia wapo vijana wengine wanahisi wakioa watakuwa wamepoteza
kabisa dira ya maisha kwasababu wanawachukilia wanawake kama kikwazo katika maisha
yao.Ila kama utaishi vizuri na mkeo hawezi kuwa kiwazo chochote katika maisha
yako.Hizo ni baadhi tu ya sababu ambazo huwa zinawafanya wanaume wengi wasioe
kabisa ila pia kwa upande wa wanawake zipo pia sababu ambazo zinawafanya
wasiolewe kabisa.Sababu mojawapo ni baadhi ya wanawake kutohitaji kabisa kuzaa
hivyo wanaona hawana sababu ya wao kuolewa na wanaamua kuishi maisha yao
binafsi.Na ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anayetaka kuoa mwanamke ambaye
hayuko tayari kumzalia watoto.Sababu ya pili ya wanawake kutoolewa ni kwamba
wanawake wengi wanahisi wakiolewa watanyanyasika kwa wanaume zao ila si mkweli
kwamba watanyanyasika iispokuwa kila mmoja anapaswa kumuheshimu mwenzie ili
waweze kwenda sawa katika maisha ambayo wameamua kuishi pamoja.Kama mtakuwa na
mtazamo tofauti basi kutofautiana kutakuwepo ila isiwe ni sababu ya kutoolewa.Pia
wanawake wengine hawaolewi kwasababu wamekuwa wakijirahisha kwa wanaume zao
kipindi wanapokuwa katika mahusiano ya awali na inafikia hatua mwanaume
anamuona hana jipya kwasababu amesha mpa kilakitu hivyo anaona hata akimuoa
hakuna cha zaidi atakachokuja kukipata maana ameshapewa vyote pindi wakiwa
katika mahusiano ya ujana,hivyo wanawake wanapaswa wajitafakari mara mbilimbli
kwa wanaume zao wasijiachie ikapitiliza.Pia wanawake wengi wamekuwa
wakihitaji kuwa huru,hawataki kubanwabanwa na wanaume zoa ndo maana
hawataki kabisa swala zima la kuolewa.Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazowafanya
wanaume wasioe na wanawake wasiolewewe.
No comments:
Post a Comment