Wednesday, 25 January 2017

JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA


JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAISHA
Zipo baadhi ya changamoto ambazo huwa zinawakabili watu kwenye jamii na inafika wakati wanakata tamaa kabisa ya maisha na wanaanza kujutia kwanini wamezaliwa.Lakini kwa binadamu aliye kamilika hana budi kupambana na izo changamoto ili kuhakikisha anafikia malengo yake aliyo kusudia katika maisha.Katika maisha hakuna kitu kibaya kama kukata tama.Unapo fikia hatua ya kukata tama maana yake ni kwamba umeishiwa mbinu za kupambana na changamoto za maisha.Kiualisia maisha ni kama wilibaro yanaenda pale ambapo wewe binafsi unayaelekeza yaende. Kama utayaelekeza kwenye kukata tama basi nayo yataelekea uko maana dereva wa iyo wilibaro ya maisha ni wewe mwenyewe.Lengo langu kubwa hasa la kuandika makala hihi ni kukuelimisha jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.Zipo baadhi ya changamoto ambazo huwa zinawakabili watu kwemye jamii ambazo ni kama vile ugumu wa maisha,ukosefu wa ajira,ukosefu wa elimu ,ukosefu wa chakula bora,malazi bora,na nyinginezo.Lakina  pamoja na kuwa na changamoto izo zote nilizozitaja hakuna mtu mwingine yeyote wakukutatulia izo changamoto isipokuwa juhudi zako binafsi na maarifa yako binafsi ndiyo yatakayo kusaidi a na kukuvusha pale ulipo kwama na kukupeleka mbele zaidi ya hapo ulipo.Nimeshawai kukutana na baadhi ya watu wamekata tama kabisa na masha na imefikia hatua wanatamani hata kujiua ili waweze kuepukana na changamoto za maisha.Lakini kiuwkeli kabisa maisha yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu na jitihada kubwa sana ili kuhakikisha unafikia malengo yako.Wapo baadhi walidhani kuwa wakisha ajiriwa watakuwa wamefanikiwa katika maisha lakini bado wameendelea kukabiliwa na changamoto za maisha,Vilevile wapo baadhi walizani wakisoma hadi chuo kikuu basi watakuwa wamemaliza changamoto za maisha kabisa,ila ukweli ni kwamba changamoto katika maisha huwa haziishi kwa asilimia mia moja isipokuwa huwa zinapungua tu kwa kiasi Fulani.Sasa kikubwa kinacho hitajika zaidi ni kutumia kile kidogo ulicho jaliwa kukipata ili uweze kukiongeza zaidi na zaidi kwasababu kama hutakitumia vizuri basi hata ukipewa kikubwa hivyo hivyo  hutaweza kukitumia..Tumia elimu yako uliyoipata kuhakikisha unatimiza ndoto zako za maisha na usiwe mtu wakulalamika maisha magumu kila wakati uku umejaliwa nguvu na mwenyenzi Mungu,huna ukilema wowote ule ambao utakuzuia wewe kupambana na changamoto za maisha.Hivyo basi tufanye kazi kwa bidii zote ili tuweze kukidhi changamoto za maisha na pia tusikate tama ya maisha tuzidi kuwa na ujasiri na tusiziogope changamoto za maisha kwasababu zipo kwa ajili yetu sisi binadamu na sio wanyama au mimea.

No comments:

Post a Comment