JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA
MAISHA
Zipo baadhi ya changamoto ambazo
huwa zinawakabili watu kwenye jamii na inafika wakati wanakata tamaa kabisa ya
maisha na wanaanza kujutia kwanini wamezaliwa.Lakini kwa binadamu aliye
kamilika hana budi kupambana na izo changamoto ili kuhakikisha anafikia malengo
yake aliyo kusudia katika maisha.Katika maisha hakuna kitu kibaya kama kukata
tama.Unapo fikia hatua ya kukata tama maana yake ni kwamba umeishiwa mbinu za
kupambana na changamoto za maisha.Kiualisia maisha ni kama wilibaro yanaenda
pale ambapo wewe binafsi unayaelekeza yaende. Kama utayaelekeza kwenye kukata
tama basi nayo yataelekea uko maana dereva wa iyo wilibaro ya maisha ni wewe
mwenyewe.Lengo langu kubwa hasa la kuandika makala hihi ni kukuelimisha jinsi
ya kukabiliana na changamoto za maisha.Zipo baadhi ya changamoto ambazo huwa
zinawakabili watu kwemye jamii ambazo ni kama vile ugumu wa maisha,ukosefu wa
ajira,ukosefu wa elimu ,ukosefu wa chakula bora,malazi bora,na
nyinginezo.Lakina pamoja na kuwa na
changamoto izo zote nilizozitaja hakuna mtu mwingine yeyote wakukutatulia izo
changamoto isipokuwa juhudi zako binafsi na maarifa yako binafsi ndiyo yatakayo
kusaidi a na kukuvusha pale ulipo kwama na kukupeleka mbele zaidi ya hapo
ulipo.Nimeshawai kukutana na baadhi ya watu wamekata tama kabisa na masha na
imefikia hatua wanatamani hata kujiua ili waweze kuepukana na changamoto za maisha.Lakini
kiuwkeli kabisa maisha yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu na jitihada kubwa
sana ili kuhakikisha unafikia malengo yako.Wapo baadhi walidhani kuwa wakisha
ajiriwa watakuwa wamefanikiwa katika maisha lakini bado wameendelea kukabiliwa
na changamoto za maisha,Vilevile wapo baadhi walizani wakisoma hadi chuo kikuu
basi watakuwa wamemaliza changamoto za maisha kabisa,ila ukweli ni kwamba
changamoto katika maisha huwa haziishi kwa asilimia mia moja isipokuwa huwa
zinapungua tu kwa kiasi Fulani.Sasa kikubwa kinacho hitajika zaidi ni kutumia
kile kidogo ulicho jaliwa kukipata ili uweze kukiongeza zaidi na zaidi
kwasababu kama hutakitumia vizuri basi hata ukipewa kikubwa hivyo hivyo hutaweza kukitumia..Tumia elimu yako
uliyoipata kuhakikisha unatimiza ndoto zako za maisha na usiwe mtu wakulalamika
maisha magumu kila wakati uku umejaliwa nguvu na mwenyenzi Mungu,huna ukilema
wowote ule ambao utakuzuia wewe kupambana na changamoto za maisha.Hivyo basi
tufanye kazi kwa bidii zote ili tuweze kukidhi changamoto za maisha na pia
tusikate tama ya maisha tuzidi kuwa na ujasiri na tusiziogope changamoto za
maisha kwasababu zipo kwa ajili yetu sisi binadamu na sio wanyama au mimea.
No comments:
Post a Comment